HABARI MPYA

Your Ad Spot

Jul 10, 2017

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita. 
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa hiyo mitatu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba 50 kwa wizara ya Afya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,  Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Anna Mkapa
 Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akiangalia hotuba yake alipokuwa hajahutubia wananchi mbalimbali katika uwanja wa michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Picha namba 
 Kikundi cha ngoma za asili cha Chato kikitumbuiza katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita
. Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe hati ya kituo cha kukamua Mafuta ya Alizeti  (Double Refine) kilichojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages