MKUU WA WILAYA YA DODOMA MJINI CHRISTINA MDEME AKUTANA NA KAMATI NDOGO YA URATIBU UJENZI WA UWANJA WA MICHEZO WA KIMATAIFA MKOANI DODOMA

 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini  Christina Mdeme akizungumza na Kamati ndogo ya Mkoa inayoratibu Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa utakojengwa katika kata ya Nala, alipokutana na Kamati hiyo ofisini kwake mjini Dodoma, leo
 Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa, Salum Mkuya akitoa mrejesho wa mambo yaliyofanywa na Kamati yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Christina Mdeme  katika kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa.
 Mjumbe wa hiyo ambaye ni Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Evordy Kyando akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mdeme  wakati Kamati hiyo ilipokutana na Mkuu huyo wa Wilaya. 

Mjumbe wa hiyo ambaye ni Afisa Tawala Wilaya ya Dodoma Hashimu Kitambuliyo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mdeme kuhusu mipango na mikakati iliyoweka na Kamati hiyo katika kufanikisha Mradi huo. (Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma)

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.