Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( kulia)
na Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen,(kushoto)
akizungumza wakati wa mafunzo ya kufunga wa migodi yanayotolewa kwa Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi.Mafunzo hayo ya siku tano yanatolewa na Serikali ya Canada jijini Dar Es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( katika waliokaa) akiwa katika picha ya
pamoja na Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi
wakati wa mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa kwa siku tano
jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada. Kushoto kwake ni Mkuu wa Maendeleo
kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen, na kulia kwake ni Afisa Rasilimali Watu
Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Suzan Kiwelu.
Washiriki wa mafunzo ya ufungaji migodi ambao ni Kamati
ya Kitaifa ya ufungaji Migodi wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo
hayo yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada.
Afisa Rasilimali Watu Mkuu kutoka Wizara ya
Nishati na Madini, Suzan Kiwelu ( kulia) na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi John
Shija( kushoto) wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku
tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada.
Wakufunzi wa mafunzo ya ufungaji migodi kutoka
nchini Canada wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa mafunzo hayo.
Na
Zuena Msuya DSM,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo amefungua mafunzo ya ufungaji
wa migodi yanayotolewa kwa wataalam wa mbalimbali wanaoshiriki katika Kamati ya
Kitaifa ya ufungaji wa Migodi.
Watalaam hao wanatoka katika Wizara na Taasisi
mbalimbali za Serikali, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kukabiliana na
changamoto zinazojitokeza wakati wa ufungaji wa migodi nchini.Mafunzo hayo
yanatolewa jijini Dar Es Salaam,na Serikali ya Canada kwa siku tano kuanzia
27-31 machi 2017.
Akizungumza wakati wa akifungua wa mafunzo hayo, Dkt.
Pallangyo alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wataalamu wa migodi nchini
kuwa na uelewa zaidi juu ya hatua zote zinazotakiwa kufuatwa wakati na baada ya
ufungaji wa migodi ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza baada ya migodi kufungwa.
Dkt. Pallangyo, alifafanua kuwa, kwakuwa Serikali ya
Canada imejikita katika Sekta ya Madini kwa zaidi ya miaka 200, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia wataalam wa ndani kufahamu
na kujifunza namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kupitia migodi iliyokwishafungwa katika nchi
hiyo ili yasijitokeze hapa nchini.
" Tusiwe watu wa kusoma tu na kufunga migodi,
tujifunze kwa vitendo kutoka kwao makosa waliofanya wakati wa ufungaji wa
migodi kwa kuwa Canada ipo katika Sekta ya madini kwa zaidi ya miaka 200 na tujirekebishe,
ili makosa yaliyotokea kwa yasijirudie katika migodi yetu," alisisitiza
Dkt.Pallangyo.
Vilevile, ameiomba
Serikali ya Canada kutoa mafunzo hayo mara kwa mara na kwa muda mrefu ili kupata
wataalam wengi zaidi na wenye uelewa mpana katika Sekta ya Madini hasa ufungaji
wa migodi hapa nchini: Mafunzo hayo yatawawezesha watalaam kubaini kodi halisi inachotakiwa
kulipwa Serikalini pamoja na njia rahisi ya utunzaji wa ardhi na mazingira kwa
ujumla.
Kwa upande wake, Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi
wa Canada, Sue Steffen aliesema kuwa nchi yake inauzoefu wa zaidi ya miaka 200
katika sekta ya madini, hivyo wameona ni busara kutoa mafunzo hayo kwa nchi
zinazoendelea na zinazochimba madini mbalimbali.
Alisema, lengo ni kutoa elimu na kuzijengea uwezo
wa kukabiliana na changamoto zilizowahi kujitokeza katika ufungaji wa migodi
nchini Canada, na hivyo kuziepusha nchi hizo katika madhara yanayoweza
kujitokeza.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mhandisi
Elizabert Nkini alisema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea uelewa zaidi katika
ufungaji wa migodi, licha kuwepo kwa vigezo vya ufungaji wa migodi hiyo lakini
uelewa umekuwa ni mdogo kutokana kutofahamu kwa vitendo changamoto nyingi.
"Migodi nchini ni muhimili mkubwa wa mapato,
lakini pia ni chanzo kikubwa cha uharibu wa mazingira, hivyo kama mazingira na ardhi yetu havitatunzwa vizuri
kabla na baada ya kuchimbwa tutaicha nchi yetu katika hali ya jangwa isiyofaa
na vyanzo vya maji vitaharibiwa, hivyo mafunzo hayo yatatuwekea utatatibu mzuri
wa kuacha mazingira yetu yakiwa salama na ardhi salama pia,". alisema
Mhandisi Nkini.
Aidha alisema kuwa elimu hiyo waliyoipata
wataifikisha kwa wananchi wanaozunguka Migodi husika ili na wao wawe na uelewa
juu ya ufungaji wa migodi kwa kufahamu taratibu na hatua mbalimbali za kufuata
kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment
ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇