MAVUNDE ATOA RAI KWA BENKI NA TAASISI ZA FEDHA KUSOGEZA HUDUMA ZAO VIJIJINI ILI KUWAHUDUMIA WAKULIMA

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde, akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki ya Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde, wa kushoto  akiwa katika uzinduzi wa benki ya Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde amezitaka benki na Taasisi za Fedha kusogeza huduma zao katika maeneo ya Vijijini ili kuwafikia watanzania wengi ambao wanajihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na Ufugaji.


Mavunde alitoa rai hiyo jana wakati wa uzinduzi wa benki ya Yetu Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro kwa kuzitaka Taasisi hizo za fedha zisaidie katika utoaji wa mikopo nafuu kwa wakulima ikiwemo mikopo ya fedha taslimu,mikopo ya zana za kilimo na mashine za uchakataji wa mazao kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kupitia uchumi wa Viwanda.


Mavunde amewataka wananchi wa kata ya Mngeta kuitumia hiyo fursa kuboresha kilimo chao kwa kulima kwa njia za kisasa na pia kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya uchakataji mazao.


Aidha,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Bwana Millinga alimuelezea Naibu waziri kwamba wameshaanza mchakato wa kuwakopesha wakulima mashine za uchakataji wa mazao na watatanua wigo zaidi ili kuwafikia wakulima wengi zaidi.


sheila simba

Posted in

Spread the love

DC TEMEKE MHE FELIX LYAVIVA AWAAGIZA WAKURUGENZI JIJINI DAR ES SALAAM KUANZISHA DAFTARI LA WAKAZI KILA MTAA

MKUU wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe Felix Lyaviva akizungumza wakati wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Mitayakingi Kilaba akitoa maelezo kuhusu semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe Felix Lyaviva akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mrakibu msaididzi wa Polisi Makao Makuu kitengo cha Makosa ya mitandao Joshua Mwangasa Akielezea takwimu na jinsi ya kudhibiti makosa ya mitandao ya kijamii nchini.
Meya wa Manispaa ya Ubungo Ndg Boniface Jacobo (Kulia) akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Katibu Tawala wa Manispaa ya Kinondoni Bi Gift Msuya akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Theresia Mbando akifatilia kwa makini semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Isaya Mwita akitoa mtazamo wake wakati wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini

Na Mathias Canal, Dar es salaam

MKUU wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam Mhe Felix Lyaviva amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa za Kigamboni, Ilala, Temeke, Kinondoni na Ubungo kuanzisha daftari la wakazi katika kila Mtaa katika Jiji la dar es salaam.

Alisema kuwa ili kupunguza uhalifu katika Mkoa wa Dar es salaam ni vyema kuwatambua wananchi wote na mahali wanapoishi ikiwemo kubaini wageni wote wanaowasili katika Jiji hilo na mahali wanapofikia.

Ametoa agizo hilo wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda katika ufunguzi wa semina ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ili kuwaelimisha watumiaji wa Intaneti wapatao milioni 20 sambamba na watumiaji wa simu za mikononi wapatao milioni 40 kuwa na matumizi bora ya simu za mikononi na mitandao ya kijamii.

Katika Semina hiyo wadau wamekumbushwa namna ya kuelewa Zaidi hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji, Umuhimu wa anuani za makazi na Post-kodi kwa maendeleo ya Taifa, Faida za huduma ya kumiliki na kuhama na namba ya simu ya kiganjani na mwelekeo wa Teknolojia na huduma za mawasiliano na utangazaji hapa nchini.

 Mhe Lyaviva alisema kuwa pamoja  na faida kubwa inayopatikana kutokana na kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini ambayo inawezesha ukuaji wa kasi wa sekta nyingine, kumekuwepo na watu wachache katika jamii ambao wanatumia fursa hiyo vibaya hivyo kusababisha usumbufu kwa watu binafsi na jamii kwa ujumla.

Alisema kuwa wapo wanaotumia simu na mitandao ya kijamii kupanga mikakati ya uhalifu huku wengine wakitumia simu na mitandao hiyo kukashifu na kutukana watu wengine.

Mhe Lyaviva alisema kuwa lengo la serikali ni kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya Mawasiliano na utangazaji ili kutoa fursa za ajira na kuwezesha huduma hizo kuwafikia wananchi wote kwa gharama nafuu.

Naye Mrakibu msaididzi wa Polisi Makao Makuu kitengo cha Makosa ya mitandao Joshua Mwangasa akiwasilisha mada kuhusu makosa ya mitandao ya kijamii alisema kuwa kuna njia nyingi zinazotumiwa ili kufanya uhalifu ikiwemo mitandao ya kijamii hivyo amewasihi watumiaji wote wa mitandao ya kijamii nchini kubadili mara kwa mara Namba za siri (Password).

Alisema kuwa kufanya hivyo ni miongoni mwa njia nzuri ya kuepuka kuingiliwa na wahalifu katika mawasiliano yao kwani kwa kiasi kikubwa maisha ya binadamu yanaenda kubadilika kutokana na teknolojia

Akitoa takwimu na jinsi ya kudhibiti makosa hayo kwa viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam, Mwangasa alisema kuwa Mwaka 2016 makosa ya mitandao ya kijamii yameongezeka kufikia 9441 ukilinganisha na Mwaka 2015, ambapo amezitaja sababu za kuongezeka kwake kuwa ni pamoja na ongezeko la uelewa wa wananchi na hatimaye kutoa taarifa za matukio hayo katika vituo mbalimbali vya Polisi nchini
sheila simba

Posted in

Spread the love

MAGAZETI YA LEO JUNE 24,2017sheila simba

Posted in

Spread the love

KAMATI YA KUDUMU YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA KUTOKA BUNGE LA MSUMBIJI YATEMBELEA OFISI ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Chomera Jeremiah (kushoto) Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015 wakati Kamati hiyo ilipotembelea Ofisi za Tume leo jijini Dar es salaam.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya Tume kwa  Wabunge wa Bunge la Msumbiji ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa waliotembelea Ofisi za NEC jijini Dar es salaam kujifunza namna Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Lucas Chomera Jeremiah na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Hamis Mkunga.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Emmanuel Kawishe (kushoto) akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji namna Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Chomera Jeremiah (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Wajumbe wa Kamati hiyo kutoka Msumbiji na watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania leo jijini Dar es salaam, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji wamezitembelea Ofisi za NEC kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala ya Uchaguzi.Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (Kulia) akisalimiana na Wabunge wa Bunge la Msumbiji na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wa nchi hiyo waliotembelea Ofisi za NEC kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa chaguzi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji waliozitembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam.  PICHA/Aron Msigwa - NEC
sheila simba

Posted in

Spread the love